Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2025

SERA YA MAENDELEO YA VIJANA TANZANIA, 2007 (TOLEO LA 2024)

 UTANGULIZI.  Mageuzi ya Sera za Vijana Tanzania yalianza miaka ya 1990 wakati wa vuguvugu la uanzishwaji wa vyama vingi nchini. Sera ya kwanza ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ilikuwa ya mwaka 1996, ikafuata ya mwaka 2007 na ya sasa 2024. Kwa takribani miaka 15 vijana wa Kitanzania wamekuwa wakiongozwa na Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana (2007) ambayo kwa namna nyingi sera hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo utekelezaji mdogo katika maeneo mbalimbali ya kisekta, vijana wengi kutofahamu uwepo wake hasa katika maeneo mengi ya vijijini, changamoto mpya za kidunia nk. Katika kipindi chote cha utekelezaji, Sera iljikita katika masuala ya maendeleo ya vijana ambayo ni pamoja na; uwezeshaji wa kiuchumi, mazingira, kukuza ajira, ushiriki wa vijana, H1V na UKIMWI, jinsia, sanaa na utamaduni, michezo, afya ya uzazi kwa vijana na masuala ya maisha ya familia nk. MAFANIKIO YA SERA YA TAIFA YA MAENDELEO YA VIJANA (2007) Kuimarika kwa ushiriki wa vijana katika uon...