UTANGULIZI.
Mageuzi ya Sera za Vijana
Tanzania yalianza miaka ya 1990 wakati wa vuguvugu la uanzishwaji wa vyama
vingi nchini. Sera ya kwanza ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ilikuwa ya mwaka
1996, ikafuata ya mwaka 2007 na ya sasa 2024.
Kwa takribani miaka 15 vijana wa
Kitanzania wamekuwa wakiongozwa na Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana (2007)
ambayo kwa namna nyingi sera hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto kadhaa
ikiwemo utekelezaji mdogo katika maeneo mbalimbali ya kisekta, vijana wengi
kutofahamu uwepo wake hasa katika maeneo mengi ya vijijini, changamoto mpya za
kidunia nk.
Katika kipindi chote cha
utekelezaji, Sera iljikita katika
masuala ya maendeleo ya vijana ambayo ni pamoja na; uwezeshaji wa kiuchumi,
mazingira, kukuza ajira, ushiriki wa vijana, H1V na UKIMWI, jinsia, sanaa na
utamaduni, michezo, afya ya uzazi kwa vijana na masuala ya maisha ya familia
nk.
MAFANIKIO YA SERA YA TAIFA YA MAENDELEO YA VIJANA (2007)
- Kuimarika kwa ushiriki wa vijana katika uongozi na tasnia ya utamaduni, sanaa na michezoKuongezeka kwa taasisi zisizo za kiserikali zinazojihusisha na masuala ya maendeleo ya vijana nchini kutoka 3,800 mwaka 2007 hadi 11,400 mwaka 2021
- Kutungwa na/au kufanyiwa marekebisho kwa Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura ya 410 na Kanuni zake za mwaka 2013
- Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, Sura ya 290.
- Kuanzishwa kwa kada ya Maendeleo ya Vijana katika ngazi ya mikoa na halmashauri ili kuratibu masuala ya vijana
- Kuanzishwa kwa mafunzo ya Shahada ya Awali ya Utawala katika Maendeleo ya Vijana na Uongozi katika Chuo Kikuu Mzumbe.
Mafanikio mengine ni;
- Kupungua kwa kiwango cha maambukizi ya VVU kutoka 2.15% mwaka 2011 hadi 0.66% mwaka 2021 kwa vijana wa umri wa miaka 15-19, na 5.55% mwaka 2011 hadi 1.0% mwaka 2023 kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15-24;
- Kupungua kwa kiwango cha mimba katika umri mdogo kutoka 24% mwaka 2010 hadi 22% mwaka 2022;
- Kutengwa kwa ekari 274,091.33 za ardhi kwa ajili ya vijana kufanya shughuli za kiuchumi ambapo zaidi ya vijana 194,553 wamenufaika.
- Kufanikisha
uanzishwaji wa makampuni 345 ya vijana wajasiriamali mwaka 2022 kutoka
makampuni 12 mwaka 2007
- Kuimarika
kwa ujumuishwaji wa vijana kwenye utekelezaji wa mifuko na programu za uwezeshaji
wananchi kiuchumi.
Licha ya mafanikio ya utekelezaji wa Sera, tathmini ya utekelezaji (2022) ilibaini kuwapo kwa upungufu kama ifuatavyo (baadhi):
i. Kukosekana kwa Mkakati wa Utekelezaji.
Sera haikuwa na mkakati wa utekelezaji suala ambalo limesababisha kutokuwepo kwa ufanisi katika utekelezaji, uratibu na ufuatiliaji wa sera hiyo.
ii. Sera Kutozingatia Baadhi ya Masuala Muhimu Yaliyoainishwa Kwenye Makubaliano na Itifaki Mbalimbali za Kikanda na Kimataifa.
Masuala hayo ni pamoja na ushiriki wa vijana katika mchakato wa kisiasa na ujenzi wa amani kwa ajili ya utulivu wa kisiasa, kijamii na kiuchumi kama ilivyobainishwa kwenye Ibara ya 8.1.5 ya Sera ya Vijana ya Afrika Mashariki (2013); Ibara ya 17 ya Mkataba wa Vijana wa Afrika (2006); Lengo Mahsusi Na. 5 la Mkakati wa Vijana wa Umoja wa Mataifa wa 2030 na Tamko la 4(13) la Agenda ya Afrika 2063; na utambuzi na uendelezaji wa vijana wavumbuzi na wabunifu kama ilivyo kwenye sehemu ya 3(b)(iii) ya Azimio la SADC Kuhusu Maendeleo na Uwezeshaji wa Vijana (2015).
iii. Baadhi ya Matamko ya Sera Kutojibu Hoja Zilizoainishwa.
Baadhi ya matamko yenye upungufu huo yapo katika maeneo ya kisera yanayohusu fasili ya kijana; vijana na ushirikiano wa kikanda na utandawazi; vijana, elimu na mafunzo; na haki za vijana. Upungufu huu unaweza kusababisha kuwekwa kwa jitihada ambazo hazitatui changamoto za vijana zilizokusudiwa na hivyo kushindwa kufikia malengo ya Sera.
Kwa uchambuzi wa kina juu ya Sera ya Vijana ya mwaka 2007, Toleo la 2024, tazama kiungo chini kwa vide:
👇👇
Comments
Post a Comment